-
Mufti wa Uganda ataka kupigwa marufuku TikTok nchini humo
Apr 01, 2025 10:39Mufti wa Uganda, Sheikh Shaaban Ramadhan Mubajje, ametoa mwito kwa serikali kuu kupiga marufuku programu ya mtandao wa kijamii wa TikTok nchini humo, ambayo anasisitiza kuwa inatumiwa na watu wasio na kazi kuwakashifu na kuwapaka matope watu wengine.
-
Jeshi la Uganda: Tumeua waasi zaidi ya 200 mashariki ya DRC
Mar 23, 2025 02:47Jeshi la Uganda limetangaza habari ya kuwaua mamia ya wapiganaji wa kundi la waasi wa CODECO baada ya kushambulia kambi ya jeshi la Uganda katika mpaka wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
WHO: Uganda imeripoti kifo kingine cha Ebola
Mar 02, 2025 12:26Shirika la Afya Duniani WHO likinukuu Wizara ya Afya ya Uganda limesema mgonjwa wa pili wa Ebola amefariki dunia katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
-
Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kuushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo
Feb 16, 2025 09:14Jenerali Muhoozi Kainerugaba Mkuu wa jeshi la Uganda jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kuwa nchi hiyo itaushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo iwapo wapiganaji wote katika eneo hilo hawatasalimisha silaha zao katika muda wa saa 24.
-
Uganda yatuma askari 1,000 zaidi mashariki mwa DRC
Feb 05, 2025 02:40Uganda imeripotiwa kutuma wanajeshi zaidi ya 1,000 wa ziada huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndani ya wiki moja iliyopita, karibu na eneo ambalo wanajeshi wa serikali ya Kinshasa wanapambana na waasi wa M23.
-
Museveni apuuza uamuzi wa mahakama juu ya mahakama za kijeshi
Feb 02, 2025 12:30Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema serikali yake itaendelea kuwashtaki raia katika mahakama za kijeshi, licha ya Mahakama ya Juu ya nchi hiyo kupiga marufuku hatua hiyo, ikisema ni kinyume cha katiba.
-
Wafuasi wa kundi lenye misimamo mikali waua, kujeruhi 16 Uganda
Oct 30, 2024 14:17Watu kadhaa wanaoshukiwa kuwa wafuasi madhehebu ya kidini yenye misimamo ya kufurutu ada wameshambulia kijiji kimoja nchini Uganda, na kuua watu wasiopungua wanane, akiwemo mtoto wa umri wa miaka mitatu na watu wa familia za washambuliaji hao.
-
Jumatano, tarehe 9 Oktoba, 2024
Oct 09, 2024 02:22Leo ni Jumatano tarehe 5 Rabiuthani 1446 Hijria inayosadifiana na Oktoba 9 mwaka 2024.
-
Maambukizo ya ugonjwa wa Mpox yaongezeka nchini Uganda
Sep 15, 2024 07:27Idadi ya wagonjwa nchini Uganda walioambukizwa aina mpya ya virusi vya Mpox imeongezeka hadi 11, huku afisa mkuu wa afya akiripoti kuwa hakuna vifo vilivyosababishwa na maradhi hayo kufikia jana Jumamosi nchini humo.
-
Mahakama ya Uganda yamkuta na hatia kiongozi wa waasi wa LRA
Aug 14, 2024 08:11Mahakama nchini Uganda jana ilimpata na hatia kamanda wa zamani wa kundi la Waasi wa Kikristo la kaskazini mwa Uganda (LRA). Thomas Kwoyelo amepatikana na hatia kwa kuhusika katika makosa kadhaa ya jinai dhidi ya binadamu katika kesi ya kwanza ya jinai za kivita kusikilizwa katika nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika.