-
Sasa ni ruhsa kwa polisi wa Uturuki kuvaa Hijabu
Aug 27, 2016 23:34Kwa mara ya kwanza, serikali ya Uturuki imetoa ruhusa kwa polisi wa kike kuvaa vazi la staha la Hijabu wakiwa kazini. Ruhusa hiyo imetolewa kupitia hukumu iliyotangazwa jana Jumamosi katika gazeti rasmi la serikali.
-
Serikali ya Damascus: Operesheni ya kijeshi ya Uturuki ndani ya ardhi ya Syria ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala
Aug 24, 2016 10:32Wizara ya Mambo ya Nje ya Syria imelaani operesheni ya kijeshi ya Uturuki iliyopewa jina la Ngao ya Euphrates huko kaskazini mwa Syria na kueleza kuwa uingiliaji huo wa kijeshi wa Ankara ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka ya kujitawala ya nchi hiyo.
-
Shambulio la bomu laua watu 50 na kujeruhi 100 harusini Uturuki
Aug 21, 2016 10:59Watu wasiopungua 50 wameuawa na wengine wapatao 100 wamejeruhiwa katika shambulio la kigaidi la kujitolea mhanga lililolenga sherehe ya harusi katika mkoa wa Gaziantep ulioko kusini mashariki mwa Uturuki.
-
Zarif na Cavusoglu wajadili masuala ya kieneo
Aug 19, 2016 12:13Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Mevlut Cavusoglu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki amekutana na kufanya mazungumzo hapa Tehran na Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kwa muda wa masaa matano.
-
Russia yasisitizia mazungumzo chanya baina yake na Iran na Uturuki kuhusu Syria
Aug 19, 2016 03:32Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesema, mazungumzo ya pande tatu yanayoendelea baina ya nchi hiyo na Iran na Uturuki kuhusu Syria ni yenye taathira chanya.
-
Safari ya Zarif Uturuki; fupi lakini ya mafanikio mengi
Aug 14, 2016 01:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Muhammad Javad Zarif, siku ya Ijumaa alifanya safari ya siku moja nchini Uturuki; safari fupi lakini iliyokuwa na mafanikio mengi. Katika safari yake hiyo Zarif alikutana na kufanya mazungumzo na waziri mwenzake wa Uturuki pamoja na Rais wa nchi hiyo.
-
Waziri Zarif afanya mazungumzo na Rais wa Uturuki mjini Ankara
Aug 12, 2016 22:21Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Muhammad Javad Zarif amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki huko mjini Ankara katika safari ya kwanza muhimu kufanywa na ujumbe wa ngazi za juu wa kigeni tangu lilipotokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi nchini humo.
-
Erdogan: Marekani ichague ima Fathullah Gulen au Uturuki
Aug 11, 2016 08:57Katika kile kinachoonekana kuendelea kuingia doa uhusiano kati ya Ankara na Washington, Rais wa Uturuki ametoa machaguo mawili kwa Marekani.
-
Velayati: Iran, Uturuki zina nafasi chanya katika ulimwengu wa Kiislamu
Jul 31, 2016 23:34Mshauri wa Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Uturuki zina nafasi muhimu katika kuboresha mustakabali wa ulimwengu wa Kiislamu.
-
Uturuki yawapiga kalamu nyekundu wanajeshi 1,400
Jul 31, 2016 11:49Uturuki imewapiga kalamu nyekundu takriban maafisa 1,400 wa jeshi la nchi hiyo, wanaotuhumiwa kuwa na uhusiano na Fethullah Gulen, raia wa nchi hiyo anayeishi Marekani anayetuhumiwa kupanga mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli.