-
Kongo yawatuhumu waasi sita kwa kuua raia
Aug 20, 2016 23:28Mahakama ya kijeshi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewatuhumu wanachama sita wa kundi la waasi wa Uganda kwa kushiriki katika mauaji wiki iliyopita, ambapo makumi ya raia waliuliwa mashariki mwa Kongo.
-
Makumi ya waasi wa ADF wakamatwa mashariki mwa Kongo
Aug 19, 2016 11:34Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa makumi ya waasi wa Uganda wamekamatwa mashariki mwa Kongo.
-
Watu 5 wauawa katika mapigano Mali, askari 5 watoweka
Aug 09, 2016 23:08Kwa akali watu watano wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano makali yaliyojiri kati kati ya Mali, huku duru za kiusalama zikiarifu kuwa askari watano wa serikali wametoweka baada ya kujiri mapigano hayo.
-
Makabiliano kati ya jeshi na wabeba silaha Nigeria yaua 19
Aug 07, 2016 08:43Watu 19 wameuawa katika makabiliano makali kati ya askari wa jeshi la serikali na kundi la wabeba silaha katika jimbo la Niger nchini Nigeria.
-
Uganda yaahidi kuisaidia DRC kupambana na waasi wa ADF
Aug 05, 2016 00:22Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameahidi kuwa serikali yake itaisaidia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kukabiliana na kundi la waasi la ADF-Nalu ambalo limekuwa tishio la muda mrefu la nchi mbili hizo jirani.
-
Waasi wa FLEC wadai kuua askari 17 wa jeshi la Angola
Aug 02, 2016 03:27Waasi wa kundi linalopigania kujitenga eneo la Cabinda nchini Angola FLEC wamedai kwamba wameua askari 17 wa nchi hiyo katika makabiliano makali yaliyojiri mwishoni mwa wiki iliyomalizika.
-
Waasi wa Uganda washambulia Beni mashariki mwa Kongo, waua watu kadhaa
Jul 31, 2016 11:48Waasi wa Uganda wameshambulia eneo la Beni huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.
-
Kuongezeka mgawanyiko wa kisiasa Sudan Kusini
Jul 25, 2016 06:48Mgawanyiko wa kisaisa umeshadidi huko Sudan Kusini kufuatia Riek Machar kiongozi wa waasi wa nchi hiyo kumfukuza Taban Deng Gai kwa upande mmoja; na matamshi ya kiwanagenzi ya Deng Gai na sisitizo lake la kusalia katika nafasi yake kwa upande wa pili.
-
Mapigano mengine yaibuka mashariki mwa Congo kati ya jeshi na waasi wa Mai-Mai
Jul 22, 2016 23:44Mapigano mapya yameripotiwa kutokea kati ya waasi wa Mai-Mai na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
39 wauawa na kujeruhiwa katika hujuma dhidi ya kambi ya jeshi Mali
Jul 20, 2016 03:01Askari 12 wa jeshi la Mali wameuawa katika shambulizi lililotekelezwa na waasi mapema jana katikati mwa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.