Jul 31, 2016 16:18 UTC
  • Waasi wa Uganda washambulia Beni mashariki mwa Kongo, waua watu kadhaa

Waasi wa Uganda wameshambulia eneo la Beni huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua watu kadhaa na kuwajeruhi wengine.

Jean Paul Paluku Nngahandondi, Mkuu wa asasi isiyo ya kiserikali ya kutetea haki za binadamu nchini humo amesema kuwa raia wawili, wanajeshi wawili wa Kongo na waasi watatu wa Uganda wameuawa katika shambulio lililofanywa na waasi wa Uganda huko Beni  mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa mwanajeshi mmoja wa jeshi la Kongo na askari jeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa pia wamejeruhiwa katika shambulio hilo la waasi wa Uganda. 

Jean Paul Paluku Nngahandondi, ameeleza kuwa hali ya utulivu katika eneo la Beni jana usiku ilirejea katika hali ya kawaida licha ya baadhi ya raia kulikimbia eneo hilo. Paluku amesisitiza juu ya ulazima wa kutekelezwa oparesheni kubwa ya jeshi kwa kushirikiana na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa ili kukomesha uwepo wa waasi huko Beni.

Eneo la Beni na maeneo ya mashariki mwa Kongo yanayoathiriwa na machafuko

Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekuwa yakisumbuliwa na hali ya mchafukoge  tangu miaka 20  iliyopita. Kushindwa jeshi la Kongo na wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja wa Mataifa kuyatokomeza makundi ya wanamgambo wenye silaha kumesababisha kuongezeka ukosefu wa amani katika maeneo hayo.  

 

Tags