Aug 19, 2016 16:04 UTC
  • Makumi ya waasi wa ADF wakamatwa mashariki mwa Kongo

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa makumi ya waasi wa Uganda wamekamatwa mashariki mwa Kongo.

Lambert Mende amesema kuwa waasi 80 wa ADF-NALU kutoka Uganda wametiwa nguvuni katika mji wa Beni mkoani Kivu Kaskazini mashariki mwa Kongo. Raia 51 waliuawa katika shambulio lililofanywa na waasi hao wa Uganda katika mji wa Beni Jumamosi usiku.  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Jumanne wiki hii alituma ujumbe huko Beni uliowajumuisha Matata Ponyo, Waziri Mkuu wa nchi hiyo na wawawakilishi kadhaa kutoka Baraza la Ulinzi la Kongo ili kuchunguza hali ya mambo katika mji huo baada ya waasi wa Uganda kufanya shambulizi na kuuwa makumi ya raia.

Waasi wa Uganda mashariki mwa Congo

Waasi wa Uganda wamekuwa wakifanya  mashambulizi na kutekeleza hujuma mbalimbali huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwezi Oktoba mwaka juzi. Waasi hao wanatuhumiwa kuwauwa raia zaidi ya 600 katika mji wa Beni.

 

Tags