-
Wakimbizi zaidi waendelea kumiminika nchini Burundi
Feb 22, 2025 23:13Idadi ya wakimbizi wanaoingia nchini Burundi kutokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inazidi kuongezeka huku juhudi za kuupatia ufumbuzi mgogoro wa mashariki mwa DRC zikiwa bado hazijazaa matunda.
-
Wamorocco waandamana dhidi ya waziri wa utawala wa Kizayuni
Feb 22, 2025 23:12Wananchi wenye hasira wa Morocco wameandamana kupinga uwepo wa Waziri wa Usafirishaji wa utawala wa Kizayuni katika kongamano la kimataifa nchini Morocco.
-
Mzozo wa DRC: Bunge la Rwanda lalaani azimio la EU dhidi yake
Feb 22, 2025 08:28Bunge la Rwanda limekosoa vikali azimio lililopasishwa hivi karibuni na Bunge la Ulaya, likidai kuwa Rwanda linahusika na mzozo na machafuko yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
China yaiambia G20: Lazima dunia iisikilize Afrika, iyape uzito masuala yanayoitia wasiwasi
Feb 22, 2025 02:25Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema, lazima dunia isikilize "kile Afrika inachosema" na kuuchukulia wasiwasi ilionao Afrika "kwa uzito". Wang ameyasema hayo katika hotuba yake mbele ya hadhara ya washiriki wa mkutano wa Kundi la Mataifa 20 (G20) unaofanyika mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini.
-
Rais wa Afrika Kusini amwalika mwenzake wa Ukraine kwa ziara ya kiserikali
Feb 21, 2025 23:39Rais Cyril Ramaphos wa Afrika Kusini amemwalika rais mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky afanye ziara ya kiserikali nchini humo.
-
Mkuu wa IEBC aliyesimamia uchaguzi wa kwanza Kenya kubatilishwa na mahakama afariki
Feb 21, 2025 07:25Wafula Wanyonyi Chebukati, aliyesimamia uchaguzi wa urais uliobatilishwa na Mahakama mwaka 2017 na 2022 ulioigawanya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ( IEBC) amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 63.
-
Rwanda: Vikwazo vya Marekani si halali, havina msingi wowote
Feb 21, 2025 03:41Serikali ya Kigali imelaani vikali hatua ya Wizara ya Hazina (Fedha) ya Marekani ya kumwekea vikwazo Waziri wa Utangamano wa Kieneo wa Rwanda, Jenerali (Mstaafu) James Kabarebe, kwa tuhuma za kuhusika na mzozo na machafuko yanayoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Jeshi la Somalia laangamizi magaidi 130 wa al-Shabaab kusini mwa nchi
Feb 21, 2025 03:21Somalia imesema jeshi la nchi hiyo likishirikiana na vikosi washirika vimefanikiwa kuzima mashambulizi ya al-Shabaab, na kuua makumi ya wanachama wa genge hilo la kigaidi.
-
Afrika Kusini: Usitishaji vita Gaza sharti ulete amani ya kudumu
Feb 20, 2025 23:20Rais wa Afrika Kusini amesema usitishaji wa mapigano katika Ukanda wa Gaza unapasa kuleta uadilifu na amani ya kudumu katika eneo hilo.
-
Wasudan wanarejea makwao licha ya kuandamwa na mashaka na matatizo
Feb 20, 2025 22:56Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Sudan wameendelea kurejea katika maeneo yao waliyoyakimbia kutokana na vita, lakini bado hofu na wasiwasi umetamalaki kwenye nyoyo zao.