-
Vyombo vya habari: Iran imetungua ndege tatu zisizo na rubani katika mji wa Esfahan
Apr 19, 2024 04:28Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran umetungua ndege tatu ndogo zisizo na rubani katika mkoa wa Esfahan ulioko katikati mwa nchi saa kadha baada ya vyombo vya habari vya Marekani kuwanukuu maafisa waandamizi wa nchi hiyo wakidai kwamba makombora ya utawala wa Kizayuni wa Israel yamepiga eneo la Iran.
-
Iran yalaani madai ya viongozi wa Ulaya na mawaziri wa fedha wa G7 dhidi yake
Apr 18, 2024 23:16Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha madai ya viongozi wa nchi za Ulaya na mawaziri wa fedha wa kundi la G7 pamoja na matamshi ya baadhi ya wakuu wa Marekani na kusema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitosita hata mara moja kujihami na kulinda maslahi yake ya kitaifa.
-
Ustawi wa biashara ya nje yenye mlingano chini ya uongozi wa serikali ya 13 ya Iran
Apr 18, 2024 23:14Kituo cha Takwimu cha Kamisheni ya Ulaya kimetangaza kuwa Katika mwezi wa kwanza wa mwaka huu wa 2024, uagizaji wa bidhaa wa Ugiriki kutoka Iran uliongezeka mara 3 na Uholanzi mara 2, nayo mauzo ya Uhispania kwa Iran yakaongezeka kwa asilimia 62 na Italia kwa asilimia 13.
-
Gharibabadi: Nchi za Magharibi ziache sera za kinafiki na ubaguzi kuhusiana na ugaidi
Apr 18, 2024 10:05Katibu wa Baraza Kuu la Haki za Kibinadamu la Iran amesema kuwa, Marekani na nchi za Magharibi kwa ujumla zinapaswa kuachana na siasa zao za kindumakuwili na ubaguzi kuhusiana na ugaidi.
-
SEPAH: Vitisho vya Israel dhidi ya Iran si vipya na Tehran muda wote iko tayari kujibu mashambulizi ya adui
Apr 18, 2024 10:00Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya nchini Iran SEPAH amesema kuwa, vitisho vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Iran haviwezi kuifanya Jamhuri ya Kiislamu kubadilisha sera na siasa zake kuhusu kustafidi kwa njia ya amani na teknolojia ya nyuklia.
-
Kukiri Pentagon kuhusu uwezo wa kijeshi wa Iran katika kuujibu utawala wa Kizayuni
Apr 18, 2024 08:49Patrick Ryder Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) amekiri juu ya nguvu za kijeshi za Iran katika kutoa jibu la kijeshi kwa utawala wa Israel.
-
Iran: Marekani ilikuwa na taarifa kuhusu Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya kuutia adabu utawala wa Israel
Apr 18, 2024 04:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema, Jamhuri ya Kiislamu iliikuwa imeshaitaarifu serikali ya Marekani kabla ya kutekeleza Operesheni ya Ahadi ya Kweli ya kuutia adabu utawala wa Israel mfanyamauaji ya kimbari.
-
Iran yapinga hukumu ya mahakama ya Argentina kuhusu mashambulizi ya mabomu
Apr 18, 2024 01:12Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kanani, ametupilia mbali uamuzi wa mahakama ya Argentina unaoilaumu Iran kwa mashambulizi mawili ya mabomu nchini humo katika muongo wa 90, na kuyataja madai katika hukumu hiyo kuwa yasiyo na ushahidi na yenye msukumo wa kisiasa.
-
Vikwazo vipya vya Marekani; muendelezo wa sera iliyofeli dhidi ya Iran
Apr 17, 2024 23:03Kufuatia kushindwa utawala wa Kizayuni na Marekani katika kukabiliana na mashambulizi ya kulipiza kisasi ya ndege zisizo na rubani na makombora ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel), Washington kwa mara nyingine inajaribu kuiwekea Iran vikwazo vipya vya silaha.
-
Kujitetea kwerevu kwa Iran kwa ajili ya Gaza
Apr 17, 2024 08:11Hatua ya Iran kujitetea kihalali dhidi ya shambulio la kichokozi la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wake nchini Syria, ambayo ilifanyika kwa utaratibu wa hali ya juu na kupitia silaha tofauti za mashambulio, imekuwa na athari na matokeo ya kieneo na kimataifa angalau imepelekea wakaazi wa Gaza kupata usiku mmoja wa amani na utulivu.