Wananchi wa Kano Nigeria waandamana kulaani jinai za Israel huko Gaza
Waislamu na waungaji mkono wa Palestina katika mji wa Kano, Nigeria wameandamana na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi madhulumu wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamelaani vikali jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya mauaji ya watoto na watu wasio na hatia wa Gaza.
Waislamu na wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria mjini Kano, wameandamana wakiwa wamebeba bendera za Palestina na kutangaza kuunga mkono muqawama wa Gaza.
Wanawake na vijana walikuwa na mahudhurio makubwa katika maandamano hayo dhidi ya utawala vamizi wa Israel na kutangaza kuwa, kuna haja kwa ulimwengu wa Kiislamu kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina hususan waa Ukanda wa Gaza.
Waislamu nchini Nigeria wamekuwa wakiandamana kila mara na kusisitiza uungaji mkono wao mkubwa kwa wananchi wa Palestina na muqawama wao dhidi ya uvamizi wa Israel na jinai zake.
Wiki iliyopita pia, Waislamu katika Jimbo la Bauchi la Nigeria walifanya maandamano wakipeperusha bendera za Palestina huku wakitoa nara za "Tunaunga mkono Hamas," "Tunaunga mkono Palestina," "Mauti kwa Israel na Mauti kkwa Marekani".
Wafuasi wa Palestina katika mji wa Kano wiki iliyopita pia waliingia barabarani kuupongeza muqawama wa kishujaa wa Wapalestina hususan operesheni ya Kimbunga cha al-Aqswa