Dec 23, 2023 06:39 UTC
  • Mwisho wa kuwepo kijeshi  Ufaransa nchini Niger, ushindi kwa Waniger

Kuwepo kijeshi Ufaransa nchini Niger kumemalizika kwa kuondoka kundi la mwisho la wanajeshi wa nchi hiyo huko Niamey mji mkuu wa Niger.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Iranpress, kundi la mwisho la wanajeshi wa Ufaransa liliondoka Ijumaa jioni katika Kambi ya 110 ya anga ya Niamey katika hafla iliyohudhuriwa na makamanda wakuu wa jeshi la Niger.

Mchakato wa kuwaondoa wanajeshi wa Ufaransa nchini  Niger ulianza Oktoba 2023.

Baada ya kuchukua uongozi serikali ya kijeshi, wananchi wa Niger kwa kujumuika na kufanya maandamano kila wiki walitaka kukomeshwa kuwepo kisiasa na kijeshi Ufaransa nchini humo ambapo siku ya Ijumaa iliashiria ushindi mkubwa wa kihistoria kwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa Ufaransa waliondoka katika nchi ya Niger kwa  ndege ya kijeshi na ya kubebea mizigo ya nchi hiyo, hivyo historia ya kisiasa ya nchi hiyo ikawa imeingia katika awamu mpya.

Serikali ya kijeshi na wananchi wa Niger daima wamekuwa wakitilia mkazo suala la kulindwa na kuhifadhiwa uhuru wa kisiasa, kijeshi na kiuchumi wa nchi yao.

Awali, watu wa Niger walisherehekea huko Niamey kuondoka kwa balozi wa Ufaransa nchini humo, na kusisitiza kuwa baada ya kupatikana ushindi wa pili, yaani, kuondoka kabisa  vikosi vya jeshi la Ufaransa, wangesherehekea ushindi wa pili nchini humo. 

Katika sherehe za kuondoka Balozi wa Ufaransa, vijana wengi wa Niger waliiambia Iranpress kuwa watu wote wa nchi hiyo watasherehekea tena wakati wa kuondoka kabisa Wafaransa nchini kwao.

Tags