Feb 05, 2024 03:15 UTC
  • Alfajiri Kumi; Uongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika njia ya Imam Khomeini (M.A)

Mtafiti na Mhadhiri wa Chuo Kikuu katika mji wa Zaria nchini Nigeria amesema kuwa, Ayatullah Khamenei anaongoza Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran katika njia sawa na ya Imam Khomeini (M.A).

Isa Hassan Mshelgaru Mhadhiri wa Chuo Kikuu katika mji wa Zaria nchini Nigeria ambaye pia ni mwandishi amehojiwa na shirika la IranPress na kueleza kuwa: Imam Khomeini amewafunza shakhsia mashuhuri mbalimbali, na sasa Kiongozi Muadhamu wa Iran Ayatullah Khamenei anaongoza vyema Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 

Mshelgaru ameeleza haya kwa mnasaba wa kukaribia maadhimisho ya miaka 45 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.  

Mtafiti huyo  mtajika wa Kiislamu katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria amesisitiza kuwa baada ya Imam Khomeini (M.A), Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yameendeleza harakati yake iliyo bora kwa kulinda  thamani za kimapinduzi katika njia ya fikra na misingi aliyoiasisi.

Imam Khomeini (M.A)

Isa Hassan Mshelgaru ameongeza kuwa: Mapinduzi ya Kiislamu ya wananchi wa Iran chini ya uongozi wa Imam Khomeini mwanafalsafa mkubwa yamevuka mipaka ya nchi hii, na maeneo mbalimbali ya dunia yamenufaika na matunda ya Mapinduzi ya Kiislamu.  

Tags