Feb 15, 2024 07:47 UTC
  • Wabunge wa Somaliland wafutilia mbali makubaliano na Ethiopia ya kufika Bahari Nyekundu

Wabunge katika eneo lililojitenga na Somalia la Somaliland wamefutilia mbali makubaliano waliyofikia na Ethiopia ya kuiruhusu Addis Ababa kutumia bandari kuu katika eneo la Somaliland.

Katika taarifa yao ya jana jioni, wabunge wote wa mabunge mawili ya Somaliland, hususan kutoka majimbo ya Adwal na Salal katika pwani ya eneo hilo, wamesema kuwa makubaliano ya Bahari Nyekundu yaliyofikiwa kati ya Somalind na Ethiopia yalikuwa kinyume cha sheria na yalikuwa na lengo la kuvuruga umoja wa watu wa Somaliland.  

Utiaji saini wa makubaliano tajwa baina ya viongozi wa Ethiopia na Somaliland

Taarifa hiyo imesema: "Tunapinga makubaliano hayo na utekelezaji wake, na tunaitaka serikali isimamishe utekelezaji wa hati ya makubaliano hayo." Taraifa ya wabunge wa mabunge ya Somaliland imeashiria taarifa zinazokinzana kutoka kwa viongozi wa Somaliland na Ethiopia kuhusu makubaliano hayo ambayo yanairuhusu Ethiopia kuwa na kituo cha kudumu cha wanamaji na huduma za baharini na kibiashara katika Ghuba ya Aden.

Somalia kwa upande wake ilipinga makubaliano hayo yaliyofikiwa mapema mwezi Januari mwaka huu kati ya Somaliland na Ethiopia kuhusu bandari katika Bahari Nyekundu na kuyataja kuwa kinyume cha sheria, na kwamba yanakiuka mamlaka yake ya kujitawala.  

Uhusiano kati ya nchi mbili hizo umekuwa mbaya tangu Ethiopia ilipofikia makubaliano na Somaliland mnamo Januari 1 mwaka huu. Serikali ya Ethiopia imetetea uamuzi wake wa kusaini makubaliano hayo bila ya kuidhinishwa na serikali ya Mogadishu ikisema kuwa kufikia makubaliano na Somaliland hakutauathiri upande au nchi yoyote,"

Tags