May 08, 2024 07:05 UTC
  • DRC na Uganda kufufua ushirikiano wao wa kijeshi

Serikali za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda zimetangaza kufufua ushirikiano wao wa kijeshi.

Hiyo ni kufuatia mkutano wa viongozi wakuu wa majeshi ya nchi hizo mbili uliofanyika katika mji wa Kasindi kwenye mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda.

Akizungumuza na makamanda wa jeshi la Congo FARDC, mkuu wa jeshi la Uganda UPDF Jenerali Kainarugaba Muhoozi amesema kuwa, Uganda haina budi kushirikiana na Congo kwani ni majirani, ndugu na marafiki wa muda mrefu.

Amesema ushirikiano ni lazima kwa nchi hizo mbili kwani zinalazimika kuwalinda raia wao dhidi ya mashambulizi ya kundi la kigaidi la ADF.

Kadhalika Mkuu wa Jeshi la Uganda UPDF Jenerali Kainarugaba Muhoozi amesisitiza kwamba, uamuzi huu ni ishara kwamba nchi hizo za Kiafrika zina uwezo wa kumaliza mgogoro wao bila ya msaada kutoka nje.

Marais wa Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (kushoto) na Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda

 

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jenerali Christian Tshiwewe Songesa amewapongeza Marais Felix Tshiskedi wa Congo na Yoweri Museveni wa Uganda kwa kuanzisha ushirikiano huo mpya baada ya Uganda kumteua kamanda mpya wa jeshi lake.

Tunapaswa kuunga mkono juhudi za viongozi wetu kwa kuweka majeshi yetu ya mataifa mawili pamoja kwa ajili ya kupambana na adui yetu ADF anaye aua raia wetu, nakushurukuru kwa uteuzi wako kuwa kiongozi mpya wa jeshi la Uganda,” amesema Jenerali Tshiwewe.

Kabla ya makubaliano hayo, jeshi la Uganda limekuwa likishutumiwa katika wilaya Rutshuru kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, jambo ambalo Uganda daima imekuwa ikikanusha.