Kiongozi wa al Qaida nchini Libya aangamizwa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11203-kiongozi_wa_al_qaida_nchini_libya_aangamizwa
Jeshi la Anga la Libya limetangaza kuwa limefanikiwa kumuangamiza kiongozi wa kundi la kigaidi la al Qaida nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 13, 2016 23:39 UTC
  • Kiongozi wa al Qaida nchini Libya aangamizwa

Jeshi la Anga la Libya limetangaza kuwa limefanikiwa kumuangamiza kiongozi wa kundi la kigaidi la al Qaida nchini humo.

Taarifa ya jeshi la Anga la Libya imesema kuwa Ibrahim al Sheikh ameuawa akiwa pamoja na wasaidizi wake watano katika eneo la Al-Raqta huko mashariki mwa mkoa wa Ajdabiya.

Ibrahim al Sheikh alikuwa kiongozi wa tawi la genge la Saraya al Difaa lililochini ya mtandao wa al Qaida. Ibrahim al Shekh alikoswakoswa kuuawa na akajeruhiwa katika shambulizi lililofanyinwa hapo awali na Jeshi la Anga la Libya katika mji wa Benghazi.

Makundi mbalimbali ya kigaidi yalitumia vibaya ombwe wa kisiasa uliojitokeza nchini Libya baada ya kuondolewa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Muammar Gaddafi na kutwaa maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.