Shirika la Nishati ya Upepo Kenya ni 'Mtu wa Mwaka wa UN'
(last modified Tue, 29 Oct 2024 02:59:31 GMT )
Oct 29, 2024 02:59 UTC
  • Shirika la Nishati ya Upepo Kenya ni 'Mtu wa Mwaka wa UN'

Kampuni ya mradi wa uzalishaji nishati ya upepo kutoka Kaunti ya Kajiado Kenya imejinyakulia tuzo ya umoja wa Mataifa nchini Kenya ya 'mtu bora wa mwaka 2024.'

Dkt. Keneth Namunje, mwenyekiti mtendaji wa kampuni ya Craftskills Wind Energy International ambayo imeshinda tuzo hiyo amesema ushindi huo  umewafanya watambue kwamba kazi yao ni muhimu na imefanikisha  lengo namba 7 la maendeleo la Umoja wa Mataifa. Aidha amesema wamejenga mtambo wa megawati 100 za nishati ili kuwasaidia wananchi kupata umeme.

Kampuni hiyo inamiliki mradi wa Kipeto unaotoa nishati ya umeme kwa kaya zaidi ya 250,000 katika eneo la Esilanke kaunti ya Kajiado.

Dr. Namunje amesema baada ya tuzo hii wanapanga kupanua wigo wa mradi kwa kuongeza megawati zingine 100 ili kusaidia kuongeza nguvu ya gridi.

Mbali ya kuwapa nishati ya umeme wananchi wa Kajiado mradi pia unawajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii.