Morocco yachapisha stempu ya Gaza kuwaunga mkono Wapalestina
(last modified Tue, 03 Dec 2024 07:15:58 GMT )
Dec 03, 2024 07:15 UTC
  • Morocco yachapisha stempu ya Gaza kuwaunga mkono Wapalestina

Idara ya posta ya Morocco imechukua hatua ya kuwaunga mkono Wapalestina dhidi ya utawala wa Kizayuni kwa kuchapisha stempu yenye anuani "Pamoja na Gaza".

Idara ya Posti ya Morocco ilichapisha maandishi yenye picha ya stempu hiyo kwenye akaunti yake kwenye mtandao wa kijamii na kutangaza katika taarifa: Imechapisha stempu maalumu yenye jina "Pamoja na Gaza" kwa ajili ya kuonyesha mshikamano na watu wa Palestina.

Tarifa hiyo aidha imesema, stempu hiyo imechapishwa kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Mshikamano na Watu wa Palestina na kusisitiza dhamira thabiti ya Morocco kwa suala la Palestina.

Stemu hiyo imechapishwa kwa ubunifu wa mpango wa pamoja wa ofisi za posta za nchi za Kiarabu, ambao uliamuliwa katika mkutano wa 27 wa Baraza la Mawaziri wa Mawasiliano na Habari wa nchi hizo Januari mwaka huu huko Abu Dhabi kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa mshikamano na wananchi wa Palestina.

Hatua ya Morocco ya kuchapisha stempu ya kuwaunga mkono Wapalestina inaweza kutathminiwa kama kubadilika msimamo wa serikali ya Rabat katika kadhia ya Palestina hasa kwa kutilia maanani kwamba, mwaka 2020 nchi hiiyo ilitia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Israel.