Wananchi wa Mauritania waandamana kulaani jinai za Israel
Wananchi wa Mauritania wameandamana na kulaani vikali mashambulio ya utawala haramu za Israel na jinai zake dhidi ya wananchi wa Ukanda wa Gaza.
Waandamanaji hao mbali na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina wamesisika wakipiga nara dhidi ya utawala haramu wa Israel pamoja na waungaji mkono wao.
Kadhalika waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wametoa mwito wa kupelekwa haraka misaada ya kibinadamu huko Gaza na Lebanon sambamba na kuchukuliwa hatua za kusitishwa mauaji na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel.
Maandamano hayo ni muendelezo wa maandamano mtawalia ambayo yamekuwa yakifanyika katika mataifa mbalimbai barani Afrika.
Katika upande mwingine, serikali za Magharibi zikiongozwa na Marekani nazo zimeonyesha kutoheshimu mipaka yoyote ya kimaadili au kisheria katika uungaji mkono wao mkubwa na usio na masharti kwa utawala wa Israel, iwe ni haki za kiraia ndani ya nchi hizo au za kimataifa.
Serikali za Magharibi hazijawahi kushughulikia kindumakuwili maafa yoyote ya kibinadamu tangu Vita vya Pili vya Dunia kama zinavyofanya sasa kuhusiana na maafa ya Ukanda wa Gaza.