Watu wa Chad wanasubiri matokeo ya uchaguzi wa bunge
Wananchi wa Chada Jumapili walishiriki katika uchaguzi wa kwanza wa bunge baada ya miaka 13, ambao serikali imeutaja uchaguzi huo kama hatua muhimu kuelekea kumaliza utawala wa kijeshi.
Upigaji kura ulimalizika saa 12:00 jioni kwa saa za nchi hiyo. Matokeo ya awali yanatarajiwa ifikapo Januari 15 na matokeo ya mwisho ifikapo Januari 31 katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya Kati ambaye aghalabu ni jangwa na yenye idadi ya watu milioni 18.
Wachad wamepigia kuwa bunge jipya, mabunge ya mikoa na mabaraza ya mitaa katika moja ya nchi maskini zaidi duniani. Upinzani ulisusia uchaguzi huo kwa madai kuwa haukuwa huru na wa haki.
Vyama vya upinzani viliwataka wapiga kura milioni nane wa Chad kususia uchaguzi ambao walisema matokeo yake yalikuwa yameamuliwa mapema.
Ususiaji huo uliwaacha wagombea wanaoegemea upande wa Rais Mahamat Idriss Deby Itno, ambaye aliletwa madarakani na jeshi mwaka 2021 na kisha kubakia madarakani katika uchaguzi wa urais mwezi Mei. Wagombea wa upinzani walilaani uchaguzi huu kama wa udanganyifu.
Deby alichapisha kwenye Facebook, picha zake akipiga kura yake katika kile alichokiita "siku ya kihistoria".
Jumamosi, Succes Masra, kiongozi wa chama cha upinzani cha Transformers, alisema: "Matokeo yaliyotengenezwa tayari yako kwenye kompyuta."
Upigaji kura unafanyika huku nchi hiyo ikikabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara ya magaidi wakufurishaji wa Boko Haram katika eneo la Ziwa Chad. Aidha hivi karibuni Chad ilibatilisha makubaliano ya kijeshi na mkoloni wa zamani Ufaransa. Halikadhalika Chad inakabiliwa na tuhuma kwamba Chad inaingilia mgogoro unaoikumba nchi jirani ya Sudan.
Deby alichukua madaraka mwaka 2021 baada ya kifo cha baba yake, ambaye alitawala nchi ya Sahel kwa miongo mitatu.