Yamkini Biya, 96, akatetea tena kiti chake urais wa Cameroon
Rais wa Cameroon, Paul Biya, alitoa hotuba yake ya mwisho wa mwaka kwa taifa, na kutoa ishara isiyo ya moja kwa moja kwamba bado ana nia ya kuendelea kuwa rais.
Biya alionya kwamba mwaka 2025 - mwaka ambao Cameroon inatarajiwa kufanya uchaguzi wa urais - umejaa changamoto, jambo ambalo lilitafsiriwa na baadhi ya wachambuzi kama pendekezo kwamba anajiona kama rais wa nchi hiyo ya Afrika ya Kati baada ya 2025.
Biya alisema alikuwa akisikiliza vilio vya wanachama wa chama chake ambao hivi karibuni wameanza kampeni ya propaganda ya kupigia debe urais wake.
Akiwa na karibu miaka 92, 40 kati ya hiyo akiwa ameitumikia nchi yake kama rais, Paul Biya anabaki kuwa mgombea pekee wa Chama cha Watu wa Cameroon kwa mujibu wa katiba ya chama hicho.
Uvumi kuhusu hali ya kiafya na mahali alipokuwa Rais Biya ulikuwa gumzo barani Afrika mwezi Oktoba mwaka jana. Hatimaye alijitokeza hadharani na kubatilisha uvumi uliokuwa umeenea.
Cameroon ipo katika eneo muhimu la kimkakati, kama lango la kuelekea Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) zisizo na ufikiaji wa bahari.