Nigeria yasifu maendeleo ya Iran
Msemaji wa Rais wa Nigeria ambaye pia ni Mshauri katika masuala ya habari amesifu na kupongeza maendeleo na mafanikio iliyoyapata Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika miaka 30 ya hivi karibuni.
Femi Adesina ameshiria safari ya hivi karibuni ya Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Nigeria na mazungumzo aliyofanya na viongozi wa nchi hiyo; na kupongeza maendeleo iliyopata Iran katika nyanja za usalama, uzalishaji, kilimo na teknolojia katika kipindi cha miaka 30 ya hivi karibuni.
Femi Adesina amebainisha kuwa serikali ya Nigeria imedhamiria kwa dhati kustafidi na tajiriba za Iran katika nyanja zilizotajwa.
Muhammad Javad Zarif Jumapili wiki hii alianza ziara yake katika nchi kadhaa za Magharibi mwa Afrika.
Baada ya kuizuru Nigeria, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amezitembelea pia Ghana na Guinea Conakry; na katika ziara zake hizo amekuwa na mazungumzo na baadhi ya viongozi wa nchi hizo. Mali ni nchi ya mwisho itakayotembelewa na Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika safari hii huko magharibi mwa Afrika.