Kenya yandelea kuchunguza chuma iliyodondoka kutoka anga za juu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121008-kenya_yandelea_kuchunguza_chuma_iliyodondoka_kutoka_anga_za_juu
Shirika la Anga za Juu la Kenya linaendelea kuchunguza chuma kubwa yenye muundo wa pete kudondoka katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo mapema wiki hii.
(last modified 2025-01-04T09:47:19+00:00 )
Jan 04, 2025 09:47 UTC
  • Kenya yandelea kuchunguza chuma iliyodondoka kutoka anga za juu

Shirika la Anga za Juu la Kenya linaendelea kuchunguza chuma kubwa yenye muundo wa pete kudondoka katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo mapema wiki hii.

Mnamo Desemba 30, kifaa hicho ambacho kinaaminika kuwa kati ya vyuma vya roketi japo hawajabaini ni roketi ya nchi gani kina upana wa karibu futi 8 (mita 2.4) na uzito wa paundi takriban kilo 453, klidondoka kutoka angani katika kijiji cha Mukuku, kaunti ya Makueni mashariki.

Julius Rotich, afisa wa polisi wa eneo hilo anasema wakati timu kutoka shirika hilo na maafisa wa usalama walipofika kwenye eneo la tukio hilo siku ya Jumatatu, "chombo hicho bado kilikuwa na joto'.

Wakati huo huo, Mamlaka ya  Nyuklia ya Kenya (KNRA) Ijumaa ilichukua udhibiti wa eneo hilo/.

Mamlaka hiyo inayoshughulikia masuala ya ulinzi wa mionzi na  usalama wa nyuklia inakusanya sampuli kutoka kwenye eneo hilo kwa ajili ya uchambuzi.

Ikiwa na vifaa mbalimbali vya kupimia mionzi, timu hiyo Ijumaa ilichunguza eneo hilo kwa siku nzima ikikusanya ushahidi wote.

Machi iliyopita, kipande kikubwa cha taka kutoka Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu kilidondoka kwenye nyumba moja huko Florida, Marekani na pia vipande kadhaa vya chuma kutoka kwa kapsuli ya SpaceX vilipatikana kwenye shamba moja nchini Kanada mwezi uliofuata.

Tukio linalofanana sana na lile la hivi karibuni nchini Kenya lilitokea India mnamo Aprili 2022, ambapo chuma kubwa yenye muundo wa pete ilidondoka katika eneo la vijijini.