Rais Ruto afanya mazungumzo na rais wa Angola João Lourenço
Rais wa Kenya, William Ruto, amekamilisha ziara fupi nchini Angola, ambapo alikutana na kufanya mazungumzo mjini Luanda na Rais João Lourenço wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Téte António, mazungumzo kati ya Rais Ruto na Rais Lourenço yalilenga masuala muhimu ya Kanda ya Maziwa Makuu na juhudi za kutatua migogoro inayoendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.
Mazungumzo hayo pia yalijikita katika mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako kundi la waasi la M23 linazidi kuwa changamoto kubwa katika eneo la Kivu Kaskazini.
Ziara hii ni hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya Angola na Kenya, hasa baada ya makubaliano yaliyosainiwa jijini Nairobi mwaka jana.
Kikao cha Ruto na Lourenco kinajari wakati ambao, Angola inajiandaa kuchukua urais wa Umoja wa Afrika mwezi ujao huku Kenya ikitafuta nafasi ya mwenyekiti kamisheni ya wa umoja huo kupitia Raila Odinga.
Rais wa Angola ambaye anahudumu kama msuluhishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika (AU) amekuwa akifanya juhudi za kuwakutanisha viongozi hao wawili ingawa tarehe mahsusi ya kukutana ana kwa ana haijatangazwa hadi sasa.