Ndege ndogo yaanguka barabarani na kuua watu watatu Malindi, Kenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121288-ndege_ndogo_yaanguka_barabarani_na_kuua_watu_watatu_malindi_kenya
Watu watatu wamefariki dunia kufuatia ajali ya kuanguka ndege ndogo katika kijiji cha Kwachocha huko Malindi kaunti ya Kilifi nchini Kenya.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 11, 2025 03:07 UTC
  • Ndege ndogo yaanguka barabarani na kuua watu watatu Malindi, Kenya

Watu watatu wamefariki dunia kufuatia ajali ya kuanguka ndege ndogo katika kijiji cha Kwachocha huko Malindi kaunti ya Kilifi nchini Kenya.

Ripoti zinasema, ndege hiyo iliyokuwa kwenye safari ya kawaida ya mafunzo, ilipata hitilafu ya kiufundi na kulazimika kutua katika barabara kuu ya Malindi-Mombasa, na kuua  mwendesha bodaboda, abiria wake na mtu mwingine aliyekuwa amesimama kando ya barabara.

Ripoti ya polisi inasema, ndege hiyo aina ya Cesna 172 ilikuwa ikitoka uwanja wa ndege wa Malindi kuelekea uwanja wa ndege wa Wilson, Nairobi ilipopata matatizo ya kiufundi.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni mwalimu wa shule ya msingi, wanabodaboda wawili na mmoja wao alichomeka kiasi kwamba hakutambuliwa.

Rubani wa ndege na wahudumu wengine akiwemo aliyekuwa akipatiwa mafunzo, waliokolewa na kukimbizwa hospitali.