Algeria: Matukio ya Gaza ni doa katika paji la uso wa ubinadamu
Mwakilishi wa Bunge la Algeria ameyataja matukio yanayojiri Ukanda wa Gaza kuwa ni doa katika paji la uso wa ubinadamu.
Rashid Zain amesema kuwa kinachojiri hivi sasa huko Gaza ni kuporomoka kimaadili nchi zinazodai kutetea haki za binadamu; hivi sasa majukumu makubwa yanapaswa kubebwa na nchi za Kiarabu hasa nchi jirani na Palestina abazo ni washirika na waungaji mkono wa Wazayuni maghasibu.
Utawala wa Israel unaendeleza jinai zake dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza katika hali ambayo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imeamuru kutiwa mbaroni Benjamin Netanyahu na Yoav Gallant Waziri Mkuu na Waziri wa zamani wa Vita wa utawala wa Kizayuni kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na kutumia njaa kama silaha ya kuwamaliza wakazi wa Ukanda wa Gaza.
Wakati huo huo, utawala wa Kizayuni umekiri kuwa licha ya kupita siku 464 za vita dhidi ya Gaza lakini umeshindwa kufikia malengo yake katika vita hivyo yaani kuiangamiza Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na kuwarejesha nyumbani wanajeshi wake wanaoshikiliwa mateka katika Ukanda wa Gaza.

Jeshi la utawala wa kizayuni lilianzisha vita na mauaji ya kimbari dhdi ya Gaza Oktoba 7 mwaka juzi kwa himaya na uungaji mkono wa pande zote wa Marekani na baadhi ya nchi nyingine za Magharibi na hadi sasa Israel imewauwa shahidi Wapalestina zaidi ya elfu 45 na kujeuhi zaidi ya laki moja na tisa.