Chama tawala Chad chakomba thuluthi mbili ya viti Bungeni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121370-chama_tawala_chad_chakomba_thuluthi_mbili_ya_viti_bungeni
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa mwezi Disemba 2024, yanaonesha kuwa, chama tawala nchini Chad kimekomba thuluthi mbili ya viti katika uchaguzi wa Bunge ambao ulisusiwa na sehemu kubwa ya vyama vya upinzani.
(last modified 2025-01-13T03:12:23+00:00 )
Jan 13, 2025 03:12 UTC
  • Chama tawala Chad chakomba thuluthi mbili ya viti Bungeni

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa mwezi Disemba 2024, yanaonesha kuwa, chama tawala nchini Chad kimekomba thuluthi mbili ya viti katika uchaguzi wa Bunge ambao ulisusiwa na sehemu kubwa ya vyama vya upinzani.

Vyombo vya habari vimetangaza habari hiyo na kusisitiza kwamba matokeo hayo ya uchaguzi wa Disemba 29 yamezidi kuitia nguvu serikali ya  Idriss Deby Itno kikatiba, ikiwa ni zaidi ya miaka mitatu tangu serikali hiyo ya mpito iingie madarakani baada ya kuuawa Rais Idriss Deby.

Chama cha Deby Itno cha Patriotic Salvation Movement, kimepata viti 124 kati ya 188 katika Bunge la Taifa. Kiwango cha ushiriki wa wananchi katika uchaguzi huo kilikuwa 51.56%.

Kura hiyo, ambayo pia ilijumuisha chaguzi za manispaa na tawala wa kieneo, ilikuwa ya kwanza kwa Chad katika kipindi cha zaidi ya mika kumi iliyopita.

Chama cha kiongozi wa upinzani Succes Masra cha Transformateurs na vyama vingine kadhaa vilisusia uchaguzi huo vikisema kuwa haukuwa na uwazi. Lakini Serikali imekanusha madai hayo. 

Hayo yamekuja huku mkoloni kizee wa Ulaya, yaani Ufaransa, imekabidhi kambi ya kijeshi iliyokuwa ikiishikilia katika mji wa Abeché nchini Chad baada ya kutimuliwa nchini humo, hilo likiwa ni pigo jingine kubwa kwa Ufaransa ambayo ilizifanya nchi za Afrika kuwa ni eneo lake la kujifaragua na kufanya inachotaka.