Mamlaka za Afrika Kusini zinakabiliwa na uchunguzi kuhusu zilivyoghulikia wachimba madini haramu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121568-mamlaka_za_afrika_kusini_zinakabiliwa_na_uchunguzi_kuhusu_zilivyoghulikia_wachimba_madini_haramu
Mamlaka za Afrika Kusini zinakabiliwa na hasira na malalamiko ya umma kutokana na jinsi zilivyoshughulikia mgogoro wa wachimbaji madini haramu walionaswa kwenye mgodi wa dhahabu uliogurwa huko Stilfontein, huku idadi ya waliofariki dunia kutokana na tukio hilo ikifikia watu 87.
(last modified 2025-01-17T23:10:37+00:00 )
Jan 17, 2025 23:10 UTC
  • Mamlaka za Afrika Kusini zinakabiliwa na uchunguzi kuhusu zilivyoghulikia wachimba madini haramu

Mamlaka za Afrika Kusini zinakabiliwa na hasira na malalamiko ya umma kutokana na jinsi zilivyoshughulikia mgogoro wa wachimbaji madini haramu walionaswa kwenye mgodi wa dhahabu uliogurwa huko Stilfontein, huku idadi ya waliofariki dunia kutokana na tukio hilo ikifikia watu 87.

Mamlaka husika huwenda zikakabiliwa na uchunguzi kwa sababu ya kukataa kwao hapo awali kuwasaidia wachimbaji madini na badala yake "kutaka kuwafurusha kwenye mgodi huo" kwa kuwakatia chakula na maji.

Wachimbaji madini hao wanashukiwa kufariki dunia kwa njaa na kukosa maji, ingawa hadi sasa sababu za vifo vyao bado hazijatangazwa rasmi.

Makundi ya kijamii yalianzisha majaribio ya uokoaji baada ya mamlaka za serikali kusema mwaka jana kuwa hazitasaidia mamia ya wachimba migodi hao kwa sababu ni "wahalifu."

Mbinu hiyo ya “kuwafurusha,” mgodini, kama ilivyoelezwa na waziri mmoja wa Baraza la Mawaziri, imelaaniwa na moja ya vyama vikuu vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini.

Polisi na wamiliki wa mgodi pia wanalaumiwa kwa kuchukua kamba na kubomoa mfumo uliokuwa ukitumiwa na wachimbaji haramu kuingia mgodini na kupeleka vifaa chini ya ardhi.

Stilfontein, Afrika Kusini

Mwaka jana, mahakama iliamuru serikali kuruhusu chakula na maji kufikishwa kwa wachimbaji hao, huku uamuzi mwingine wa mahakama uliotolewa wiki jana ukiilazimisha kuanzisha operesheni ya uokoaji.

Chama cha pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini, ambacho ni sehemu ya muungano wa serikali, kimemtaka Rais Cyril Ramaphosa kuanzisha uchunguzi huru kuhusu mkasa huo ambao hadi sasa umesababisha vifo vya watu wasiopuiungua 87.

Wachimba madini haramu, wanaojulikana kama "zama zamas", wanafanya kazi katika migodi iliyogurwa na sekta ya madini inayodorora ya Afrika Kusini. Watu hao wanafanya kazi bila vibali, mara nyingi katika hali na mazingira hatari, ili kuchimba mabaki ya dhahabu. Shughuli zao zimezua ukosoaji kwa madai kwamba zinachochea mitandao ya uhalifu na kuzidisha jinai katika maeneo jirani.