Afrika ilikuwa na zaidi ya miripuko 200 ya magonjwa mwaka 2024
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i121584-afrika_ilikuwa_na_zaidi_ya_miripuko_200_ya_magonjwa_mwaka_2024
Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) vimeonya kuhusu ongezeko kubwa la dharura la afya ya umma katika bara zima la Afrika, huku zaidi ya miripuko ya magonjwa 200 ikiripotiwa mwaka jana.
(last modified 2025-01-18T03:14:01+00:00 )
Jan 18, 2025 03:14 UTC
  • Afrika ilikuwa na zaidi ya miripuko 200 ya magonjwa mwaka 2024

Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) vimeonya kuhusu ongezeko kubwa la dharura la afya ya umma katika bara zima la Afrika, huku zaidi ya miripuko ya magonjwa 200 ikiripotiwa mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa CDC barani Afrika, Jean Kaseya, amesema hayo wakati akihutubia mkutano wa kuchunguza mripuko wa ugonjwa wa mpox katika nchi nyingi na majanga mengine ya kiafya na kusisitizia haja ya kufanyika haraka juhudi za pamoja za kukabiliana na dharura za afya ya umma.

Amesema: “Tunaona miripuko ya magonjwa kwa mwaka 2024 ilikuwa zaidi ya ile ya mwaka 2023... Mwaka 2024 tulikuwa na matukio 213 waka mwaka 2023 tulikuwa na 166... tunatarajia mwaka huu itakuwa tofauti na mwaka jana.”

Mkuu huyo wa Afrika CDC amebainisha kwamba magonjwa kama kipindupindu, surua, dengue, mpox na kuharisha ndiyo magonjwa ya miripuko yaliyokuwa na kesi nyingi zaidi barana Afrika kwa mwaka jana 2024.

Kipindupindu kilikuwa "muuaji nambari moja barani Afrika," kwani bara la Afrika liliripoti kese 204,115 za kipindupindu na vifo vya 3,747 mwaka jana. Surua ilifuatia kwa karibu kwa kuwa na kesi 234,320 na vifo 3,220 mwaka 2024.

Mpox alishika nafasi ya tatu kwa kusababisha vifo vingi barani Afrika kati ya magonjwa matano yenye yalilyosababisha vifo vingi barani humo mwaka 2024. 

Kaseya amesisitizia haja kubwa ya Afrika kushughulikia dharura za afya ya umma kwa ufanisi zaidi, akitoa mfano wa athari za mabadiliko ya hali ya hewa, ukuaji wa miji na mambo mengine yanayoleta changamoto kubwa.