Wanajeshi wa Ufaransa kuondoka pia Senegal
Serikali ya Ufaransa inapanga kufunga kambi yake ya kijeshi nchini Senegal baada ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Senegal.
Vyombo vya habari vya Senegal viliripoti siku ya Ijumaa, vikinukuu chanzo cha jeshi la Ufaransa, kwamba nchi hiyo inapanga kufunga kambi zake za kudumu za kijeshi huko Senegal ifikapo msimu wa joto mwaka huu.
Chanzo hiki chenye ufahamu wa kutosha kimetangaza kuwa Ufaransa iko mbioni kufanya mazungumzo ya kuondoa vikosi vyake kutoka Senegal.
Kulingana na chanzo hiki cha kijeshi cha Ufaransa, katika kiangazi cha mwaka huu wa 2025, Ufaransa haitakuwa tena na kambi ya kudumu ya kijeshi nchini Senegal.
Rais wa Senegal alithibitisha mwishoni mwa Disemba kwamba nchi hiyo inapanga kuwaondoa wanajeshi wote wa kigeni walioko nchini humo ifikapo mapema mwaka huu.
Mnamo 2023, Ufaransa iliondoa wanajeshi wake kutoka Burkina Faso na Niger kwa ombi la viongozi wa nchi hizo. Mwishoni mwa Novemba 2024, Wizara ya Mambo ya Nje ya Chad ilitangaza mwisho wa ushirikiano wa kijeshi wa nchi hiyo na Ufaransa.