Al Burhan: Makundi yanayoliunga mkono jeshi hayatanyakua mamlaka baada ya vita
Mkuu wa Baraza la Utawala na Kamanda wa Jeshi la Sudan, Abdel Fattah al-Burhan, amesema kuwa makundi yanayoliunga mkono jeshi hayatanyakua madaraka baada ya vita vya ndani nchini humo.
Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya kuwekewa vikwazo na Marekani, Al-Burhan amesema katika mkutano wake na waandishi wa habari, wasanii na wanariadha huko Omdurman kwamba: "Sikusumbua nafsi yangu kusoma maandishi ya uamuzi wa Marekani, na sina akaunti ya benki ya kigeni au mali isiyohamishika, na hata akaunti yangu ya ndani katika Benki ya Omdurman inatumika kwa ajili ya kupokea mshahara wangu kama afisa mwingine yeyote wa jeshi."
Al Burhan ameahidi kutoruhusu ushindi wa watu wa Sudan kutekwa nyara na kundi moja la watu, na kwamba makundi yanayoliunga mkono jeshi hayatahodhi madaraka ya nchi baada ya vita, akisisitiza kuwa vikosi vya kijeshi vinasimama katika safu moja na makundi mengine.
Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan ameongeza kuwa: "Hakuna nafasi kwa wanamgambo wa RSF na wale wanaowaunga mkono katika mustakabali wa nchi. Chaguo letu ni kukomboa ardhi yote ya Sudan na kuwafukuza waasi hao na wafuasi wao wa kisiasa."
Amesisitiza kwamba "watu wa Sudan wanakabiliwa na njama ya makundi ya kisiasa yanayofanya kazi kwa maslahi ya mataifa ya kigeni.