Nigeria yageukia Akili Mnemba (AI) ili kukabiliana na taarifa za uongo na kukuza lugha za ndani
Huku Akili Mnemba (AI) ikiendelea kuhuhisha sekta ya viwanda kote duniani, Nigeria nchi iliyo na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika imeamua kukumbatia kwa kasi wimbi hili la kiteknolojia.
Ingawa zana na suhula za Akili Mnemba hazikamilishi nafasi ya kazi ya binadamu ipasavyo, lakini zinazidi kutumiwa kurahisisha michakato, kazi, na kukabiliana na changamoto kama vile habari za uongo na upakiaji wa data kupita kiasi.
Nchini Nigeria, Akili Mnemba sasa inatumiwa na taasisi nyingi za habari ili kukabiliana na upotoshaji wa taarifa hasa katika majukwaa ya mitandao ya kijamii kama WhatsApp na Telegram ambako mara nyingi maudhui mbalimbali husambazwa katika mitandao hiyo bila kupitiwa na kuhakikiwa.
Temilade Onilede, Meneja wa Mradi wa Dubawa yaani Mkakati wa Kuchunguza Ukweli katika Mitandao ya Kijamii wa Afrika Magharibi amesema: "Taarifa potofu zinaenea sana kwenye majukwaa kama WhatsApp na Telegram, ambapo ni ngumu kufuatilia kile kinachoshirikiwa.
Mbali na Dubawa, taasisi nyingine za Nigeria pia zinatumia AI kuboresha ukaguzi na uandishi sahihi wa habari.