Mripuko wa Ebola: Kesi kumi na moja zathibitishwa nchini Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i131246-mripuko_wa_ebola_kesi_kumi_na_moja_zathibitishwa_nchini_kongo
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakabiliana na mripuko mpya wa ugonjwa wa Ebola, huku maafisa wa afya wakithibitisha kesi kumi na moja za ziada katika Ukanda wa Afya wa Bulape katika Mkoa wa Kasai.
(last modified 2025-10-18T05:48:37+00:00 )
Sep 26, 2025 02:29 UTC
  • Mripuko wa Ebola: Kesi kumi na moja zathibitishwa nchini Kongo

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inakabiliana na mripuko mpya wa ugonjwa wa Ebola, huku maafisa wa afya wakithibitisha kesi kumi na moja za ziada katika Ukanda wa Afya wa Bulape katika Mkoa wa Kasai.

Mripuko wa homa ya Ebola umesalia kujikita katika maeneo sita yaliyotajwa kwa majina Bambalaie, Bulape, Bulape Communautaire, Dikolo, Ingongo na Mpianga. 

Tangu tarehe 21 mwezi huu wa Septemba, jumla ya wagonjwa walioripotiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola wameongezeka na kufikia 57. Mlipuko wa Ebola hadi sasa umeuawa watu 35 .

Watoto wachanga na watu wenye umri hadi miaka 65  ni miongoni kwa walioathiriwa na Ebola. Makundi makuu yaliyo katika hatari ya kupatwa na homa ya Ebola ni pamoja na watoto, watunza nyumba, na wakulima.

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa Barani Afrika wiki iliyopita kiliripoti kuwa mlipuko wa Ebola umesababisha vifo visivyopungua 16 na kesi shukiwa 68 tangu mlipuko huo ulipotangazwa kwa mara ya kwanza mapema mwezi huu huko Bulape. 

Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vinavyojulikana kitaalam kama (Ebola Virus). Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa yajulikanayo kwa ujumla kama Homa za virusi zinazosababisha kutoka damu sehemu za wazi za mwili mfano puani , masikioni na machoni. Ugonjwa huu unaathiri binadamu na wanyawa kama vile nyani , ngedere, sokwe na popo.