Rais Pezeshkian: Iran inalenga kuimarisha uhusiano na Oman
Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu uhusiano imara kati ya Iran na Oman, na kueleza kuwa Tehran ina imani kwamba uhusiano wa pande mbili utaendelea kukua kwa "nguvu na uthabiti.
Rais Pezeshkian alisema jana wakati wa kupokea hati za utambulisho za Sayyid Yaarub bin Qahtan bin Nasser Albusaidi, Balozi mpya wa Oman nchini Iran kwamba , kuna kiwango cha juu cha "maelewano, uhusiano, na ushirikiano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Oman.
Amesema nchi mbili zinatilia mkazo haja ya kuimarisha na kupanua zaidi ushirikiano huu kuliko hapo awali.
Rais Masoud Pezeshkian ameashiria ziara yake ya karibuni huko Muscat mji mkuu wa Oman na kusema makubaliano muhimu na yenye manufaa yalifikiwa kati ya nchi mbili akiwa ziarani nchini humo.
Amesema nchi mbili zimejitolea kutekeleza makubaliano haya na kuyafuatilia.
Kwa upande wake, Albusaidi amesema "Sultan wa Oman anasisitiza sana kudumisha uhusiano imara na nchi rafikina ndugu ya Iran Iran amani, utulivu na ustawi.