Wamorocco waandamana kuunga mkono Palestina na kulaani mzingiro Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i132944-wamorocco_waandamana_kuunga_mkono_palestina_na_kulaani_mzingiro_gaza
Maelfu ya wananchi wa Morocco wameingia mitaani na kushiriki maandamano ya kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, sanjari na kulaani mzingiro dhidi ya Gaza na njama za Israel za kukwamisha upelekaji misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.
(last modified 2025-11-08T10:44:40+00:00 )
Nov 08, 2025 10:32 UTC
  • Wamorocco waandamana kuunga mkono Palestina na kulaani mzingiro dhidi ya Gaza
    Wamorocco waandamana kuunga mkono Palestina na kulaani mzingiro dhidi ya Gaza

Maelfu ya wananchi wa Morocco wameingia mitaani na kushiriki maandamano ya kutangaza mshikamano wao na wananchi wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, sanjari na kulaani mzingiro dhidi ya Gaza na njama za Israel za kukwamisha upelekaji misaada ya kibinadamu katika ukanda huo.

Maandamano hayo yaliyomefanyika chini ya kaulimbiu ya "kuendelea vuguvugu la watu wa Morocco la kupinga vita vya mauaji ya kimbari, kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel" yaliiitishwa na Kundi la Action for Palestine.

Huku wakitoa nara za kuunga mkono kadhia ya Palestina na kulaani mashambulizi dhidi ya raia, washiriki wa maandamano hayo waliitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua kukomesha ukiukaji wa usitishaji vita unaofanywa na utawala ghasibu unaokalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Washiriki wa maandamano hayo wakiwa wamebeba picha za Msikiti wa al-Aqswa na bendera za Palestina, walipiga nara za kulaani jinai za jeshi la Kizayuni katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa ukamishaji wa kutumwa misaada ya kibinadamu katika ukanda huo unaofanywa na utawala huo haramu.

Maandamano dhidi ya Israel nchini Morocco yameshika kasi katika miaka michache iliyopita hususan tangu kuanza Vita vya Gaza na jinai kubwa zinazofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina wasio na ulinzi. Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, wananchi wa Morocco mbali na kulaani jinai za Israel dhidi ya Wapalestina, mara kadhaa wametoa mwito wa kufutwa makubaliano ya kuwa na uhusiano na utawala wa Kizayuni.