Je, Nigeria iliwezaje kusambaratisha mahesabu ya mapinduzi nchini Benin?
Uingiliaji wa haraka wa Nigeria kwa ombi la serikali ya Benin, ulifelisha jaribio la mapinduzi na kuzuia kuenea kwa ukosefu wa utulivu katika Afrika Magharibi.
Kulingana na Pars Today, mapinduzi yaliyofeli nchini Benin mnamo Desemba 7, 2025, haikuwa tu mtihani kwa serikali ya Patrice Talon, lakini hilo lilibadilika na jukwaa la Nigeria kuchukua jukumu; jukumu ambalo Al Jazeera ililiona kuwa la maamuzi kutoka masaa ya kwanza ya shida.
Al Jazeera iliripoti ikunukuu ofisi ya rais wa Nigeria, kwamba serikali ya Talon iliomba mara mbili msaada wa haraka kutoka Abuja: kwanza kwa "msaada wa dharura wa anga" na kisha kwa kutumwa askari wa ardhini.
Maombi haya yalitumwa wakati kundi la wanajeshi wakiongozwa na Kanali Pascal Tigri walipochukua udhibiti wa televisheni ya taifa na kutaka rais aondolewe na kusimamishwa kazi kwa taasisi zote za kidemokrasia.
Sababu za Nigeria kuingia katika mgogoro wa mapinduzi ya Benin
Sababu ya kwanza na rasmi ya kuingilia kati Nigeria ilikuwa ombi la moja kwa moja kutoka kwa serikali ya Benin. Tovuti ya Nigeria Premium Times pia ilithibitisha kwamba serikali ya Benin iliiomba Nigeria katika maelezo mawili rasmi kuchukua hatua haraka na kuchukua udhibiti wa anga ya nchi hiyo "ili kulinda utaratibu wa kikatiba na usalama wa watu."
Nigeria, kwa amri ya Rais Bola Tinubu, ilituma ndege zake za kivita katika anga ya Benin na, kama Al Jazeera ilivyoripoti, "ilichukua udhibiti wa anga," na hivyo kuwawekea kikomo cha uwezo waliopanga mapinduzi ya kuendesha na kuratibu mambo.
Hatua hii ilikuwa na nafasi muhimu hususan katika kurejesha televisheni ya taifa na kambi muhimu ambapo waliopanga mapinduzi walikuwa wamejipanga upya.
Lakini uingiliaji kati wa Nigeria haukuwa tu jibu kwa ombi rasmi; vipimo vya kijiografia na kisiasa pia vilikuwa muhimu. Kama gazeti la Guardian lilivyobaini, Benin, tofauti na majirani zake wengi, ilikuwa na historia ya utulivu wa kiasi, na mapinduzi yake ya mwisho yaliyofanikiwa yalifanyika 1972.
Lakini eneo la Afrika Magharibi limeshuhudia mfululizo wa mapinduzi katika miaka ya hivi karibuni katika nchi jirani na Benin kuanzia Niger na Burkina Faso hadi Mali na Guinea.
Ni kwa sababu hii ndio maana, utulivu wa Benin unahesabiwa kuwa suala la usalama na kikanda kwa Nigeria. Nigeria insingeweza kuruhusu "athari hii" kufikia mipaka yake ya magharibi, ambayo yenyewe inakabiliwa na matatizo ya usalama na harakati za makundi yenye silaha.
Katika ripoti ya The Guardian imeashiriwa kwamba waliopanga mapinduzi walikuwa wametaja "hali mbaya ya usalama kaskazini mwa Benin" katika ujumbe wao wa televisheni. Kuporomoka kwa utulivu wa kisiasa nchini Benin kungeweza kuwa na athari za haraka hasi kwa mpaka na usalama wa Nigeria.
Kwa upande mwingine, Nigeria, kama mwenyekiti wa zamu wa ECOWAS (Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi) na yenye nguvu kubwa zaidi katika eneo hilo, ina jukumu la kisiasa la kutetea utaratibu wa katiba wa nchi wanachama.
Hili liliakisiwa katika taarifa rasmi za Nigeria na katika ripoti ya tovuti ya Premium Times ya Nigeria: Operesheni ya kijeshi ya Nigeria ilifanywa "kwa mujibu wa itifaki ya ECOWAS kuhusu demokrasia na utawala bora." Hakika, Tinubu, katika matamshi yake baada ya utulivu kurejea, alisema kwa uwazi kwamba vikosi vya Nigeria vilichukua hatua "kwa mwaliko wa serikali ya Benin na ndani ya mfumo wa sheria za kikanda."
Mbinu iliyotumika kutekeleza uingiliaji kati
Njia ya utekelezaji inaonyesha kwamba Nigeria ilichagua mkakati wa kasi wa kudhibiti anga ili kuzuia mapinduzi yasifanyike. Premium Times na Al Jazeera ziliripoti kwamba Nigeria kwanza ilichukua udhibiti wa anga ya Benin na kusambaza ndege za kivita ili kutatiza mawasiliano na njia za kukutana wapanga mapinduzi.
Kisha, baada ya kupokea ombi la pili kutoka Benin, vikosi vya ardhini vya Nigeria viliingia nchini humo, lakini, kama vyanzo mbalimbali vilivyosisitiza, wote walikuwa wakifanya kazi "chini ya amri ya serikali ya Benin" na dhamira yao ilikuwa ni kulinda taasisi za serikali na kuunga mkono vikosi tiifu kwa Rais Talon.
Vikosi hivihivi, pamoja na jeshi la Benin, viliweza kuondoa upinzani wa mwisho wa wapangaji mapinduzi uliotawanyika kwenye televisheni ya taifa na katika kambi zilizotajwa.
Kwa nini uingiliaji kati huu ulikuwa muhimu kisiasa kwa Nigeria?
Kwa upande mmoja, Nigeria ilitaka kutuma ujumbe wa wazi kwa wanajeshi wa kikanda kwamba zama za mapinduzi yasiyo na gharama zilikuwa zimekwisha. Kwa upande mwingine, wachambuzi wa mambo wanaamini kwamba, hali ya kisiasa ndani ya Benin, ikiwa ni pamoja na majadiliano juu ya mageuzi ya katiba, kutopasishwa mgombea wa upinzani, na uchaguzi wa rais unaokaribia, umesababisha hali ya kutokuwa na utulivu.
Nigeria iliona uingiliaji kati wake kama njia ya kuzuia Benin kuingia kwenye mgogoro wa muda mrefu, ambao kwa hakika upeo wake ungeenea nje ya mipaka ya nchi hiyo.
Kwa jumla, kile ambacho Nigeria imefanya ni mchanganyiko wa "jibu la haraka kwa mwaliko rasmi kutoka kwa nchi jirani, masuala ya usalama, jukumu la kijiografia na dhamira ya kikanda."
Wapangaji wa mapinduzi waliweza tu kutangaza ujumbe wao kwenye televisheni ya taifa kwa saa chache, na kwa mujibu wa simulizi ya pamoja ya Al Jazeera, Premium Times, na Guardian, uingiliaji kati wa haraka wa Nigeria ndio sababu iliyoizuia Benin kukariri uzoefu wa nchi jirani na kuzama katika kinamasi cha ukosefu wa utulivu.