RSF: Israel ni muuaji mkuu wa waandishi wa habari duniani
Shirika la Waandishi wa Habari Bila Mipaka (RSF) limesema utawala wa Israel ni muuaji mkuu wa waandishi wa habari duniani kwa mwaka wa tatu mfululizo, na limeutaka utawala huo uwajibike kwa kusababisha karibu nusu ya vifo vya waandishi wa habari duniani mwaka 2025, hasa katika Ukanda wa Gaza unaozingirwa.
Katika ripoti yake ya kila mwaka iliyotolewa Jumanne, RSF ilisema waandishi wa habari 29 wa Kipalestina waliuawa na jeshi la Israel huko Gaza, na kufanya asilimia kubwa ya vifo vya waandishi wa habari 67 waliouawa mwaka huu duniani kote.
Taasisi hii ya uhuru wa vyombo vya habari imesema kuwa kwa mwaka wa tatu mfululizo, Israel imekuwa tishio kubwa zaidi kwa waandishi wa habari duniani.
Tangu Israel ilipoanzisha vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya Gaza mnamo Oktoba 2023, waandishi wa habari karibu 220 wameuawa, ikithibitisha rekodi mbaya ya Israel kama muuaji mkuu wa wafanyakazi wa vyombo vya habari duniani.
Ripoti ya RSF, ambayo ilichunguza vifo vya waandishi wa habari kwa kipindi cha miezi 12 kuanzia Desemba 2024, ilibaini kuwa vikosi vya Israel vinahusika na asilimia 43 ya vifo vya waandishi wa habari mwaka huu, na kuvitaja kama "adui mkubwa wa waandishi wa habari."
RSF imesema: "Karibu nusu (43%) ya waandishi wa habari waliouawa katika miezi 12 iliyopita waliuawa Gaza na vikosi vya Israel."
Shambulio la kutisha lilitokea tarehe 25 Agosti, ambapo shambulio la aina ya "double-tap" dhidi ya hospitali katika eneo la kusini mwa Gaza liliua waandishi wa habari watano.
Israel imekuwa ikiwaita waandishi wa habari wengi wa Kipalestina kama magaidi, huku RSF ikiripoti kwamba utawala wa Israel umeanzisha kampeni ya kumchafua waandishi wa habari wa Gaza, ikiwa ni pamoja na kuwapa lebo za kifo.
Waandishi wa habari wa kigeni bado wanazuizi kubwa kuingia katika eneo lililoathirika na vita la Gaza, wakiwa wamezuiliwa katika ziara zinazodhibitiwa na jeshi la Israel, licha ya wito wa mara kwa mara kutoka kwa vikundi vya uhuru wa vyombo vya habari kwa ufikiaji huru.
Mnamo Oktoba 1, RSF ilisema lilikuwa limefungua kesi mpya, ya tano tangu kuanza kwa vita vya kimbari vya utawala wa Israel, kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kuhusiana na mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari huko Gaza.