Kutangazwa muda wa kujiuzulu Rais Omar al Bashir wa Sudan
(last modified Mon, 22 Aug 2016 08:02:01 GMT )
Aug 22, 2016 08:02 UTC
  • Rais Omar al Bashir wa Sudan
    Rais Omar al Bashir wa Sudan

Rais Omar al Bashir wa Sudan ametangaza kuwa, ana nia ya kuachia madaraka ifikapo mwaka 2020. Amesema atalazimika kuachana na siasa kwani katiba ya Sudan haitomruhusu kubakia madarakani.

Rais wa Sudan ameongeza kuwa, hana nia kamwe ya kuifanyia marekebisho katiba kwa ajili ya kubakia madarakani. Rais al Bashir amekuwa akiitawala Sudan kwa zaidi ya miaka 20 sasa, na kama alivyosema mwenyewe, wananchi wa Sudan wanataka damu mpya iingine madarakani. Hata hivyo baadhi ya wataalamu wa mambo wana wasiwasi na matamshi hayo ya Rais al Bashir na wanaaminikuwa ameyatoa kipropaganda kwa kwa ajili ya kuwafumba macho watu. Matamshi hayo ya al Bashir yametolewa huku ikiwa imebakia miaka minne hadi kufikia wakati wa uchaguzi mwingine. Inavyoonekana ni kuwa, al Bashir ametoa matamshi hayo kipropaganda kwa ajili ya kupunguza malalamiko na kukabiliana na hatari ya kupungua umaarufu wake. Omar al Bashir aliingia madarakani mwaka 1993 nchini Sudan. Tab'an kama wanavyofanya madikteta wengi wa Afrika, mara zote wanahakikisha wanaendelea kubakia madarakani kwa njia yoyote ile na hasa kupitia kuzifanyia mabadiliko katiba.

Rais al Bashir akiwa katika moja ya kampeni zake

 

Weledi wa mambo wanaamini kuwa, lengo la al Bashir la kutangaza nia yake ya kukabidhi madaraka kwa kiongozi mwingine, ni kuwavunja nguvu wapinzani wake wanaolalamikia siasa zake. Aidha jambo hilo linatoa fursa kwa wafuasi wa al Bashir kujiimarisha zaidi katika kampeni zao za kuhakikisha anaendelea kutawala, kwani tangazo hilo limelotolewa ikiwa imebakia miaka minne hadi kumailizika kipindi cha hivi sasa cha uongozi wa Rais al Bashir, na muda huo unatosha kufanyia kampeni hizo. Hivi sasa idadi kubwa ya wasomi, wanasiasa mashuhuri na watu wenye nguvu za kiuchumi katika mji wa Khartoum na eneo la katikati mwa Sudan wanaiunga mkono serikali kutokana na kupewa nafasi katika uongozi na hata wanajeshi na vikosi vingine vya usalama viko pamoja na serikali licha ya kuwa na mitazamo tofauti za kiaidiolojia. Kinachowahofisha watu hao ni kwamba kama muundo wa utawala utabadilika nchini Sudan, basi watapoteza mambo yao mengi. Watu wa daraja la kati ambao wamenufaika na ustawi wa kiuchumi na kuongezeka pato la mafuta, nao wanaona ni hatari kwao kuondoka madarakani Rais al Abashir. Ijapokuwa baadhi ya watu hao wanahisi hatari kutokana na mgogoro wa hivi sasa wa kiuchumi nchini Sdan, lakini wengi wao bado wanaiunga mkono serikali.

Khartoum, mji mkuu wa Sudan

 

Wafuatiliaji wa masuala ya Sudan wanaamini kuwa, watu wengi nchini Sudan wameizoea serikali ya hivi sasa. Serikali hiyo imeweka mlingano mzuri wa mdaraka katika sekta na taasisi mbalimbali kama vile za kijeshi, za wanaharakati wa Kiislamu na taasisi za kijamii. Inaonekana wazi kuwa Rais Omar al Bashir anatumia jambo hilo kama ngao yake ya kukabiliana na upinzani na machafuko ya aina yoyote ile nchini Sudan.

Tags