Rwanda yatahadharisha magaidi, yaua washukiwa 4
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i13795-rwanda_yatahadharisha_magaidi_yaua_washukiwa_4
Vyombo vya usalama nchini Rwanda vimesema havitafumbia macho yeyote atakayejaribu kujihusisha na mambo ya ugaidi kwa lengo la kuhatarisha usalama na amani ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 23, 2016 01:41 UTC
  • Rwanda yatahadharisha magaidi, yaua washukiwa 4

Vyombo vya usalama nchini Rwanda vimesema havitafumbia macho yeyote atakayejaribu kujihusisha na mambo ya ugaidi kwa lengo la kuhatarisha usalama na amani ya nchi hiyo.

Hii ni baada ya polisi ya Rwanda kuwaua watu wanne waliokuwa wakishukiwa kujihusisha na mambo ya ugaidi.

Watu hao wanne waliuawa na polisi katika matukio mawili tofauti huku mahakama za nchi hiyo zikiendelea kusikiliza kesi za watu wengine kadhaa zinazohusiana na ugaidi. Mauaji hayo yaliyotokea mwishoni mwa juma kwa namna fulani yanaonekana kuzua wasiwasi kwamba sasa mambo ya ugaidi yanainyemelea nchi hiyo.

Akizungumza mara baada ya tukio hilo lililotokea mjini Rusizi karibu na mpaka wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mufti Mkuu wa Rwanda Sheikh Salim Hitimana amesema mambo haya hayakubaliki na yanachafua jina la Uislamu.

Mufti Mkuu wa Rwanda amesema: Waislamu kwa kauli moja wanapinga na kulaani ugaidi na ndiyo maana wanashirikiana na polisi kutokomeza ugaidi.   

Mufti Mkuu wa Rwanda Sheikh Salim Hitimana 

Polisi ya Rwanda imesema baada ya kuwapiga risasi watu hao ambao walikuwa sita lakini wakauawa wanne miongoni kwamba iko tayari kukabiliana na yeyote atakayetaka kulipiza kisasi.

Waziri wa Usalama wa Taifa wa Rwanda, Seikh Musa Fadhil Harelimana amesema serikali haitalegeza msimamo katika suala hilo. Waziri Harelimana amesema Rwanda iko tayari kulinda usalama wa wananchi na haitakubali hata kidogo kupoteza usalama wa watu wetu.

Mpaka sasa zaidi ya watu 20 wanaendelea kusikiliza kesi zao mahakamani zenye mahusiano na ugaidi.