WHO latiwa wasiwasi na kuenea Kipindupindu Kongo DR
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa indhari juu ya kuenea ugonjwa wa kipindupindu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
WHO limeeleza wasiwasi lilionao kuhusu maambukizi ya kipindupindu nchini Kongo DR baada ya watu wapato 15,000 kukumbwa na ugonjwa huo tangu ulipoanza mwaka huu wa 2016 hadi sasa.
Eugene Kabamba, Mkuu wa masuala ya habari wa Shirika la Afya Duniani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuenea nchini humo na idadi ya watu waliokumbwa na ugonjwa huo tangu ulipoanza mwaka huu hadi sasa imeshapindukia 15,000.
Aidha ameongeza kuwa vifo 382 vimerekodiwa vya watu waliofariki kutokana na athari za ugonjwa wa kipindupindu.
Mbali na eneo la Mto Kongo, ugonjwa wa kipindupindu unaendelea kuenea pia katika mkoa wa Nord Ubangi kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.../