Makundi mawili ya wanamgambo nchini Kongo DR yaafikiana kurejesha amani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14125-makundi_mawili_ya_wanamgambo_nchini_kongo_dr_yaafikiana_kurejesha_amani
Makundi mawili ya wanamgambo kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameahidi kusaidia hatua za kurejesha amani nchini humo.
(last modified 2026-04-29T03:42:39+00:00 )
Aug 28, 2016 03:27 UTC
  • Makundi mawili ya wanamgambo nchini Kongo DR yaafikiana kurejesha amani

Makundi mawili ya wanamgambo kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameahidi kusaidia hatua za kurejesha amani nchini humo.

Muungano wa makundi yanayobeba silaha mashariki mwa Kongo DR uitwao "Umoja wa Wazalendo wa Kongo Huru na Inayojitawala" na kundi la wanamgambo wa Mai Mai yanayoendesha harakati zao katika maeneo ya kaskazaini mashariki mwa nchi yamesaini hati ya makubaliano na kuahidi kufanya jitihada za kurejesha amani na utulivu katika eneo hilo.

Kongo DR

Makundi hayo aidha yameahidi kuchukua hatua ili kukomesha mapigano na machafuko na kuondoa vizuizi vinavyokwamisha harakati za watu kuingia na kutoka huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano hayo ilifanyika jana katika mji wa Muganga, katika mkoa wenye machafuko wa Kivu ya Kaskazini chini ya usimamizi wa wabunge wa mkoa huo.

Wanamgambo wa Mai Mai

Hitilafu za kugombania umiliki wa vyanzo vya madini na ardhi na ushindani wa baadhi ya madola ya eneo, zinatajwa kuwa sababu kuu za mapigano na migogoro katika eneo hilo.

Kwa mwaka wa 20 sasa, maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yamekuwa uwanja wa vita na mapigano makali yanayohusisha makundi kadhaa ya wanamgambo katika maeneo hayo.../