Harakati ya Machi 23: Mazungumzo ya kitaifa ya Kongo hayatazaa matunda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i14839-harakati_ya_machi_23_mazungumzo_ya_kitaifa_ya_kongo_hayatazaa_matunda
Harakati ya Machi 23 ya nchini Kongo imeeleza kuwa kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini humo hakutasaidia kutatua matatizo yaliyopo.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 07, 2016 23:15 UTC
  • Harakati ya Machi 23: Mazungumzo ya kitaifa ya Kongo hayatazaa matunda

Harakati ya Machi 23 ya nchini Kongo imeeleza kuwa kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini humo hakutasaidia kutatua matatizo yaliyopo.

Bertrand Bisimwa Mkuu wa Harakati ya Machi 23 amesema kuwa mazungumzo ya kitaifa ambayo yanaendelea kufanyika huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa minajili ya kutatua mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo hayatakuwa jibu kwa changamoto kubwa zinazolikabili eneo la mashariki mwa nchi hiyo. Bertrand Bisimwa ameongeza kuwa mazungumzo ya kitaifa ya Kongo hayatasaidia kupatikana utatuzi wa matatizo ya kiusalama yanayoikabili Kongo.

Pamoja na kuwa harakati hiyo ya zamani ya waasi wa Machi 23 ilipata pigo baada ya kupigana vita kwa miezi 18 katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,hata hivyo mkoa huo na maeneo mengine ya mashariki mwa Kongo yanaendelea kushuhudia mapigano na ukosefu wa amani.

Mazungumzo ya kitaifa ya Kongo yalianza tarehe Mosi mwezi huu katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika na pasina kuhudhuriwa na shakhsia wengi wanaompinga Rais Joseph Kabila.

Rais Joseph Kabila wa Kongo DR ambaye wapinzani wanataka ang'atuke madarakani