UN yasikitishwa na ukandamizaji wa polisi nchini Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15352-un_yasikitishwa_na_ukandamizaji_wa_polisi_nchini_kongo
Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu namna jeshi la polisi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linavyowakamdamiza wapinzani nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 15, 2016 02:53 UTC
  • José María Aranaz, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
    José María Aranaz, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Umoja wa Mataifa umeelezea wasiwasi wake kuhusu namna jeshi la polisi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linavyowakamdamiza wapinzani nchini humo.

Shirika la habari la Ufaransa limenukuu José María Aranaz, mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akisema jana kwamba, kitendo cha jeshi la polisi la nchi hiyo cha kutumia silaha za mauaji kudhibiti maandamano ya wapinzani wa serikali ni jambo linalotia wasiwasi mkubwa.

Amesema, watu wasiopungua saba waliuliwa na polisi katika maandamano ya wapinzani yaliyofanyika siku ya Ijumaa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maandamano mjini Kinshasa, DRC

 

Ijumaa iliyopita watu wengi waliandamana katika mji wa Kasumbalesa kwenye mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia ili kulalamikia kuongezeka vitendo vya kihalifu na ukosefu wa usalama katika mji huo. Hata hivyo vikosi vya kulinda usalama vya serikali ya Kongo vimeripotiwa kutumia nguvu kupita kiasi kukandamiza maandamano hayo.

Maeneo ya mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hayajawahi kushuhudia utulivu na usalama kwa miaka 20 sasa.