Oct 01, 2016 07:58 UTC
  • Waasi wa FLEC wadai kuua askari 18 wa jeshi la Angola

Waasi wa kundi linalopigania kujitenga eneo la Cabinda nchini Angola (FLEC) wamedai kwamba wameua askari 18 wa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na kundi hilo imedai kuwa, waasi wa FLEC waliwaua askari hao wa jeshi la Angola katika makabiliano yaliyojiri wiki hii katika kitongoji cha Makumeni, Manispaa ya Buco Zau, muda mfupi baada ya balozi wa Ureno kulitembelea eneo hilo.

Waasi wa FLEC

Taarifa ya FLEC imewatahadharisha wananchi na jamii ya kimataifa dhidi ya kutoutembelea mkoa wa Cabinda na kusisitiza kuwa eneo hilo ni uwanja wa wamapambano na atakayeuzuru atakuwa anahatarisha maisha yake.

Ni vyema kukumbusha kuwa, mapema mwezi Agosti mwaka huu, waasi wa FLEC walidai kwamba wameua askari 17 wa nchi hiyo katika makabiliano makali yaliyojiri karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Aidha mwezi Machi mwaka huu 2016, kundi hilo la waasi lilidai kuwa limeua askari 30 wa Angola kwa kuwafyatulia risasi katika mkoa huo.

Kundi hilo ni moja ya makundi matatu ya wapiganaji wa msituni ambayo yanapigania kujitenga kwa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabinda kutoka serikali kuu ya Angola.

Tags