Mlipuko wa bomu waua watatu Blue Sky, Mogadishu
Gari lililokuwa limetegwa bomu limeripuka katika mgahawa mmoja mjini Mogadishu huko Somalia na mashahidi wanasema watu wasiopungua watatu wameuawa.
Wakazi wa Mogadishu karibu na eneo hilo la mgahawa wa Blue Sky wameeleza kuwa, mgahawa huo ambao umeshambuliwa kwa mripuko unatumiwa mara kwa mara na askari usalama wa jeshi la taifa la Somalia.
Abdifatar Omar Msemaji wa serikali za mitaa wa Somalia amethibitisha kuuawa watu watatu na kujeruhiwa wengine wanne katika mripuko huo. Wakati huo huo Sheikh Abdiasis Abu Musab, Msemaji wa oparesheni za kijeshi wa kundi la al Shabab amesema kuwa kundi hilo limehusika na shambulio hilo la leo huko Mogadishu. Ameongeza kuwa, kundi hil lilitaka kuwashambulia wafanyakazi wa seli moja iiliyo karibu na mgahawa wa Blue Sky kwa jina la Jilaow; ambako wanamgambo wa al Shabab hushikiliwa mara kwa mara.