Mamia ya wakimbizi DRC wanahitajia misaada ya dharura
Zaidi ya wakimbizi elfu moja wa kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanahitajia misaada ya haraka ya dharura.
Mkuu wa mji wa Bambesa katika jimbo la Oriantale la kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, karibu wakimbili elfu moja na 500 wamekusanyika kwenye eneo hilo tangu mwishoni mwa mwaka 2015 hadi hivi sasa, wakihitaji midaa ya haraka.
Alfred Bongwalanga ameongeza kuwa, ijapokuwa maafisa wa kutoa misaada wa mji huo wameomba kupewa misaada ya kuwasaidia wakimibizi hayo, lakini hadi hivi sasa misaada hiyo haijatolewa.
Amesema, wengi wa wakimbizi hao wamekimbilia katika mji wa Bambesa tangu mwezi Novemba na Disemba 2015 kutokana na kuongezeka mapigano katika maeneo yao.
Wakimbizi hao wamekimbia mashambulizi ya waasi wa Mai-Mai Simba na mashambulizi ya kikatili ya waasi wa ADF wa Uganda, huko Kivu Kaskazini.
Kwa upande wake, ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Bunia, makao makuu ya jimbo la Ituri, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeahidi kufikisha kilio cha wakimbizi hao kwa maafisa wa juu wa misaada, ili wafanye haraka kuwafikishia misaada wakimbizi hao wanaoishi katikamazingira magumu sana.