Umoja wa Afrika (AU) watilia mkazo kurejeshwa amani ya kudumu Somalia
Kikosi cha kudumisha amani cha Umoja wa Afrika huko Somalia (AMISOM) kimesisitiza kuhusu sualal la kurejesha amani ya kudumu katika maeneo yote ya nchi hiyo.
Kikosi hicho maalumu cha Umoja wa Afrika kilichoko Somalia kwa madhumuni ya kudumisha hali ya usalama katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo, kitakuwa na jukumu la kutoa mafunzo kwa polisi wa nchi hiyo wakati wa kufanyika uchaguzi katika eneo linalojitawala la Jubaland. Uchaguzi wa bunge nchini Somalia umeakhirishwa mara mbili mtawalia katika miezi mitatu ya hivi karibuni sambamba na kuongezeka vitisho vya kundi la al Shabab. Omar Mohammed Abdulle Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Somalia amesisitiza kuwa uchaguzi wa Rais utafanyika kama ilivyopangwa tarehe 30 mwezi Oktoba.
Mkuu wa Tume ya Uchaguzi ya Somalia amewatolea wito shakhsiya wote wa kisiasa na vile vile taasisi za kimataifa kufanya juhudi ili uchaguzi ufanyike kwa amani na kwa ushiriki mkubwa wa wananchi.