Feb 26, 2016 16:17 UTC
  • Ban: Mkataba wa amani Sudan Kusini utekelezwe

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito wa kutekelezwa mapatano ya amani Sudan Kusini.

Akizungumza Alhamisi akiwa mjini Juba, Sudan Kusini, Ban amesema pande hasimu nchini humo hazina chaguo lingine ila kuheshimu mkataba wa amani.

Ban amekutana pia na kufanya mazungumzo ya faragha na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ambaye kwa mujibu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo UNMISS ameahidi kutekeleza makubaliano ya amani. Aidha alifanya mazungumzo ya simu na kiongozi wa upinzani Riek Machar ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuwa makamu mpya wa rais.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekutana pia na wafanyakazi wa umoja huo nchini humo pamoja na mabalozi, akiwahimiza kuongeza bidii kwa ajili ya amani na usaidizi wa kibinadamu ili kupunguza machungu kwa raia wasio na hatia na akaongeza kuwa Umoja wa Mataifa utatoa dola milioni 21 kutoka katika mfuko wake wa dharura kwa ajili ya watu wa Sudan Kusini.

Tags