Umoja wa Mataifa watahadharisha kuhusu mgogoro wa kibinadamu nchini Swaziland
Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa maelfu ya watu nchini Swaziland wako katika hatari ya kukumbwa na baa la njaa kutokana na nchi hiyo kuathiriwa na uhaba mkubwa wa chakula uliosababishwa na ukame mkubwa uliotokana na el Nino.
Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephen Dujarric amesema kuwa, ukame uliotokana na mabadiliko ya tabia nchi ya el Nino huko Swaziland umesababisha watu wasiopungua laki tatu yaani moja ya tatu ya jamii ya nchi hiyo kuhitajia msaada wa dharura wa kibinadamu.
Dujarric ameongeza kuwa, hatari ya kuenea magonjwa balimbali na lishe duni imeongezeka huko Swaziland kutokana na nchi hiyo kuathiriwa na uhaba wa maji na kuwepo huduma za kiafya zisizoridhisha.
Nchi nyingine kama Lesotho, Malawi, Afrika Kusini na Zimbabwe pia zinafanya kila linalowezekana kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutokana na kuwa nchi hizo pia zimekumbwa na uhaba mkubwa wa chakula na maji.