Boko Haram yaua watu zaidi ya 1500 nchini Cameroon
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21295-boko_haram_yaua_watu_zaidi_ya_1500_nchini_cameroon
Watu zaidi ya 1500 wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram huko Cameroon.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 12, 2016 14:17 UTC
  •  Boko Haram yaua watu zaidi ya 1500 nchini Cameroon

Watu zaidi ya 1500 wameuawa katika mashambulizi ya wanamgambo wa kitakfiri wa Boko Haram huko Cameroon.

Issa Tchiroma Bakary Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon ametangaza kuwa wanajeshi na raia wa kawaida wa Cameroon zaidi ya 1500 wameuawa katika mashambulizi ya kundi la Boko Haram tangu miaka mitatu iliyopita hadi sasa. 

Kundi la kigaidi la Boko Haram mwaka 2014 lilianza kuishambulia Cameroon  kwa lengo la kuasisi utawala ulio chini yake; mashambulizi ambayo yamekabiliwa na radiamali ya muungano wa kijeshi wa Nigeria, Niger, Chad pamoja na  Cameroon yenyewe.

Nchi za eneo la Ziwa Chad zilizoathirwia na mashambulizi ya Boko Haram 

Kundi la Boko Haram lingali linaendeleza mashambulizi na milipuko ya mabomu katika maeneo mbalimbali  huko Cameroon, khususan katika mkoa wa kaskazini mwa nchi hiyo. Umoja wa Mataifa umeripoti kuwa Cameroon ni nchi ya pili baada ya Nigeria iliyoathiriwa na mgogoro wa Ziwa Chad uliosababishwa na magaidi wa kitakfiri wa Boko Haram.