Idadi ya vifo yaongezeka Kongo DR, risasi zarindima hapa na pale
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21898-idadi_ya_vifo_yaongezeka_kongo_dr_risasi_zarindima_hapa_na_pale
Milio ya risasi ya hapa na pale ilisikika Jumatano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku moja baada ya watu 26 kuripotiwa kuuawa katika maandamano dhidi ya Rais Kabila baada ya muhula wake wa uongozi kumalizika.
(last modified 2026-05-06T11:35:21+00:00 )
Dec 21, 2016 23:36 UTC
  • Idadi ya vifo yaongezeka Kongo DR, risasi zarindima hapa na pale

Milio ya risasi ya hapa na pale ilisikika Jumatano nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku moja baada ya watu 26 kuripotiwa kuuawa katika maandamano dhidi ya Rais Kabila baada ya muhula wake wa uongozi kumalizika.

Viongozi wa Kiafrika na wa nchi za Magharibi wanahofia mgogoro wa kisiasa wa Kongo DR unaweza kuwa mgogoro mkubwa na hivyo kukaririwa vita kama vile vilivyoiathiri Kongo kati ya mwaka 1996 na 2003. Mamilioni ya watu waliuawa katika vita hivyo na kupelekea nchi kadhaa jirani kutuma wanajeshi wake huko Kongo kudumisha amani.

Itakumbukwa kuwa, makabiliano kati ya waandamanaji na polisi yaliibuka mapema siku ya Jumanne, muda mfupi baada ya kumalizika muhula wa kusalia madarakani Rais Joseph Kabila.

Rais Joseph Kabila anayeshinikizwa na wapinzani aondoke madarakani 

Ripoti zinasema kuwa watu 26 wameuawa hadi sasa katika makabiliano hayo. Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch lenye makao yake mjini New York Marekani limesema kuwa watu 26 wameuawa kufikia sasa. Samy Badibanga Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu, na vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuamiliana vizuri na raia katika juhudi zao za kuimarisha usalama na amani.