Wabunge wapya wa Bunge la taifa la Somalia waapishwa mjini Mogadishu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22285-wabunge_wapya_wa_bunge_la_taifa_la_somalia_waapishwa_mjini_mogadishu
Wabunge wapya wa Bunge la taifa la Somalia wameapishwa katika hafla iliyofanyika mjini Mogadishu chini ya hatua kali za kiusalama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 28, 2016 04:39 UTC
  • Wabunge wapya wa Bunge la taifa la Somalia waapishwa mjini Mogadishu

Wabunge wapya wa Bunge la taifa la Somalia wameapishwa katika hafla iliyofanyika mjini Mogadishu chini ya hatua kali za kiusalama.

Wabunge wapya 284 wa Somalia waliapishwa jana baada ya wiki kadhaa za upigaji kura wa kuwachagua wawakilishi wapya wa Bunge la nchi hiyo ya Pembe ya Afrika inayokabiliwa na ukosefu wa usalama na amani.

Pamoja na zoezi hilo la kuwaapishwa Wabunge kufanyika jana, lakini bado baadhi ya maeneo ya nchi hiyo hayajapata wawakilishi wake kutokana na kutokamilika kwa zoei la uchaguzi huo. Kuapishwa Wabunge hao kunatajwa kuwa hatua muhimu ya kuelekea kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo ambaye kwa kawaida huchaguliwa na wawakilishi wa Bunge.

Wanamgambo wa kigaidi wa al-Shabab

Hivi karibuni serikali ya Somalia ilitangaza kuakhirishwa tena uchaguzi huo wa Rais. Uchaguzi wa Rais nchini Somalia uliokuwa umepangwa kufanyika Jumatano ya leo tarehe 28.

Afisa mmoja wa serikali ya Somalia ambaye hakutaka kutajwa jina lake aliziambia duru za habari kwamba, uchaguzi huo umeakhirishwa na kwamba kuna uwezekano tarehe nyingine ya kufanyika uchaguzi ikawa ni 24 Januari mwakani.

Somalia ambayo inafanya juhudi za kukarabati uharibifu wa miongo kadhaa iliyopita, inakabiliwa na mashambulizi ya wanamgambo wa kundi hatari la kigaidi na kitakfiri la al-Shabab ambalo limehatarisha pia usalama hata katika nchi jirani.