Umoja wa Ulaya kupunguza misaada yake kwa AMISOM
Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa utapunguza misaada yake ya kifedha kwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM nchini Somalia.
Tangazo hilo la Umoja wa Ulaya limetolewa wakati kikosi cha AMISOM kikitaka kuwepo ushirikiano mkubwa zaidi huko Somalia. Umoja wa Ulaya umesema utapunguza asilimia 20 ya misaada yake kwa kikosi hicho.
Rais huru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa tangazo hilo la Umoja wa Ulaya linavunja moyo kwa kutilia maana kwamba nchi za Afrika zinasabilia maisha ya askari wao kwa ajili ya kurejesha amani na usalama Somalia.
Askari elfu 22 wa Afrika walitumwa nchini Somalia miaka 9 iliyopita kwa ajili ya kurejesha amani na kukabiliana na kundi la kigaidi la al Shabab.
Mfuko wa kusaidia amani barani Afrika unaosimamiwa wa Umoja wa Ulaya katika kipindi cha miaka 9 iliyopita umechangia uro zaidi ya bilioni moja kwa ajili ya bajeti ya matumizi ya AMISOM.